Kuhusu PPF

Historia ya Mfuko wa PPF

Mfuko wa Pensheni wa PPF ni moja ya Mifuko ya muda mrefu uliopo kwenye sekta ya Hifadhi ya Jamii Tanzania bara. Mfuko ulianzishwa mwezi Julai 1978 chini ya kifungu cha 6 (1) cha sheria ya Mfumo wa Pensheni wa PPF (yaani PPF Pensions Scheme Act) (CAP 372 R.E. 2002) ukiwa na lengo kuu la kutoa mafao ya uzeeni kwa wastaafu na mafao ya aina nyingine kwa wanachama wanaofanya kazi kwenye sekta iliyo rasmi na isiyo rasmi pia.

 

Mabadiliko ya Jina na Chapa

 

Sheria ya Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (yaani The Social Security Regulatory Authority Act) ya Na. 8 ya 2008, ilipelekea kufanyika kwa mabadiliko kwenye jina letu la zamani lililokuwa likijulikana kama ‘’Mfuko wa Pensheni wa Mashirikia ya Umma’’ na kuwa ‘’Mfuko wa Pensheni wa PPF’’ ili kuweza kutanua wigo wa uandikishaji wanachama.

 

Aidha, chapa yetu mpya inaonyesha kiwango cha ushindani na mabadiliko yaliyopo sokoni na dhamira yetu ya kutimiza ahadi kwa kutoa mafao yanayozingatia ubunifu na utumiaji wa teknolojia sambamba na utoaji huduma kwa wateja zenye viwango vya kimataifa kutoka kwenye timu yenye uzoefu wa kutosha inayotumia teknolojia ya kisasa zaidi.

 

DIRA

Kuwa Mfuko wa kuigwa katika utoaji huduma mbalimbali za hifadhi ya jamii.

DHIMA

Kutoa pensheni, mafao na huduma nyingine za hifadhi ya jamii kwa wanachama kupitia utumiaji mzuri wa rasilimali watu na teknolojia ya kisasa pamoja na kiwango kikubwa cha umakini na kwa haraka.