QUICK LINKS
TRADITIONAL BENEFITS
Fao la Uzazi
Vigezo vya kujiunga:
- Mwanachama lazima awe mwanamke mwenye umri wa zaidi ya miaka 18
- Hutolewa kwa mwanachama mwanamke aliyejifungua mtoto/watoto kila baada ya miaka 3
- Mwanachama awe amechangia kwa kipindi cha mwaka 1 (miezi 12) mfululizo kabla ya kujifungua
- Mwanachama awe amechangia kwa kipindi kisichopungua miaka 2 (miezi 24)
Mpango wa malipo:
- Mwanachama atalipwa kiasi cha Tsh 1,000,000 mara baada ya kujifungua salama
- Malipo haya yatalipwa hadi mara 4 kila baada ya miaka 3 mara tu mama anapojifungua.
- Inapotokea mtoto amepoteza maisha ndani ya miezi 12 tokea kuzaliwa kwake, mwanachama ataweza kupata mafao yake bila ya kusubiri hadi miaka 3 ipite.
Fomu zinazohitajika:
- Fomu ya madai ya PPF iliyojazwa kwa usahihi
- Barua iliyothibithishwa na mwajiri wako kutoka kwa hospitali ambayo mwanachama anapata huduma za cliniki
- Nakala ya cheti kilichothibishwa cha kuzaliwa kwa mtoto (yaani Tangazo la kuzaliwa kwa mtoto)