Uzeeni

Sifa Zinazohitajika

  • Mwanachama awe ameondoka katika ajira amechangia katika Mfuko kwa kipindi kisichopungua mieazi 180,
  • Sababu ya kuondoka katika ajira inaweza ikawa ni kufikisha umri wa kustaafu (miaka 55-60), kupunguzwa kazini, kustaafishwa kwamanufaa ya umma au kuondolewa katika ajira na Mamlaka iliyokuweka katika ajira hiyo.

Taratibu za Utoaji wa Mafao ya Uzeeni kwa Mwanachama

  • Mafao ya mkupuo hutolewa kwa mwanachama mara anapoondoka katika ajira
  • Mafao ya uzeeni ya kila mwezi hutolewa kwa mwanachama mwenye sifa zote kama ilivyoainishwa hapo juu, Mafao ya uzeeni ya kila mwezi hutolewa kwa mwanachama hadi anapofariki.
  • Mafao ya uzeeni ya kila mwezi  yamehakikishwa kwa muda wa miezi 36. Endapo mwanachama atafariki ndani ya miezi 36 tangu aanze kupata mafao haya, PPf itaendelea kutoa mafao haya kwa wategemezi wa mwanachama aliye fariki kwa miezi iliyobakia ili kuwa na jumla ya miezi 36. Endapo mwanachama atafariki baada ya miezi 36 tangu aanze kupata mafao haya, PPF itaendelela kutoa mafao haya.

Nyaraka zinazohitajika/zinazotumika katika Mafao ya Uzeeni

  • Fomu ya madai ya mafao iliyojazwa na mwajiri
  • Maelezo kutoka kwa mwajiri kuonyesha maamuzi ya kumpunguza, kumstaafisha au kumwondoa kaika kazi ajira mwanachama
  • Picha mbili za mwanachama (pasipoti)
  • Maelezo ya Benki- Jina na akaunti, kwa ajili ya kuwekewa mfao ya uzeeni ya kila mwezi.